Pete Arredondo
MKUU wa Polisi, Pete Arredondo aliyetuhumiwa kwa kutochukua hatua stahiki katika tukio la mauaji ya wanafunzi 19 na walimu wawili huko Uvalde, katika Jimbo la Texas, amefukuzwa kazi nchini Marekani.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya bodi ya shule kupiga kura kwa kauli moja ya kumfukuza kazi Arredondo ambaye alikuwa likizo tangu Juni mwaka huu.
Shangwe zilisikika katika ukumbi huku bodi ya wadhamini wa Shule ya Robb Elementary ikiwasilisha hoja ya kumwondoa kwenye wadhifa wake mara moja.
Shambulio la mauaji ya Wanafunzi na Walimu lilitokea Mei 24, mwaka huu katika Shule ya Msingi ya Robb Elementary
Taarifa iliyotolewa na mawakili wa mkuu huyo wa polisi inaeleza kuwa Arredondo alikuwa hamjui mtu yeyote aliyekuwa ndani ya madarasa kisha kufyatua risasi.
Tukio la mauaji ya wanafunzi na walimu limetokea miezi mitatu iliyopita ambapo ilikuwa ni kabla ya wiki mbili muhula mpya wa shule kuanza.
Shambulio hilo limetokea Mei 24, mwaka huu katika Shule ya Msingi ya Robb Elementary na kwamba lilikuwa tukio baya zaidi la ufyatuaji risasi kuwahi kutokea nchini Marekani.
Askari Polisi wakliwa katika eneo la tukio
Wazazi wengi waliokuwa wahanga wa tukio hilo wameonesha kukerwa sana na mwitikio wa polisi nchini humo hivyo kumekuwa na shinikizo la kutaka vyombo vya sheria kuwawajibisha polisi.
Arredondo alikosolewa vikali kutokana na kuchelewa kwa maafisa kwa dakika 77 ili kumkabili kijana huyo mwenye bunduki na ndiye afisa wa kwanza kufukuzwa kazi.
Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao