Balozi wa Tanzania Nchini Saudi Arabia, Ali Mwadini akizungumza katika Kikao na wawekezaji kutoka nchini Saudi Arabiakilichofanyika leo Agosti 11,2022 katika ofisi za TIC jijini Dar Es Salaam.
**************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
NCHI ya Saudi Arabia imewekeza nchini Tanzania katika Miradi 13 ambayo inagharimu kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 55.2 katima Sekta ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi na kutoa ajira nyingi kwa vijana.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Revocatus Rasheli wakati walipokuwa na Kikao na wawekezaji kutoka nchini Saudi Arabia jijini Dar Es Salaam leo Agosti 11, 2022. Amesema Wawekezaji hao pia watawekeza katika Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.
Amesema TIC katika kutekeleza mkakati wa miaka mitano wa tatu wameweka kipaumbele kwenye Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ambapo wako katika kuongeza Viwango vya uzalishaji katika maeneo hayo.
Amesema kuwa wawekezaji hao wameweza kukutana na wadau kutoka bodi ya Nafaka na mazao Mchanganyiko (CPB) pamoja na Ranchi ya Taifa (NARCO) ili kuelezana kinagaubaga maeneo ambayo wawekezaji hao wanaweza kuwekeza.
Kwa Upande wa Balozi wa Tanzania Nchini Saudi Arabia, Ali Mwadini ametoa wito kwa watanzania kuwa waaminifu katika ufanyaji biashara zinazoenda nje ya nchi.
Amesema uanimifu unaweza kukuhifadhia mteja wa bidhaa na ukimfanyia visivyo utampoteza. Na lazima kila mfanyabiashara afanye kwa uaminifu asiwaangushe watanzania wengine katika biashara.
Amesema wanaweza kuzingatia Ujazo wa bidhaa ingawa bidhaa zinagombaniwa na masoko mengine, Ubora wa bidhaa lazima zizalishwe kwa ubora pia uchakataji, Usafirishaji, uhifadhi pamoja na ufungashaji lazima ufanywe kwa ubora.
Kwa upande wa mahitaji ya bidhaa za bidhaa za kilimo, Ufugaji na Uvuvi amesema hayana ukomo kwa nchi ya Saudi Arabia kwank haiwezi kuzalisha bidhaa na kujaza soko la nchi hiyo.
"Hapa Tanzania hakuna kitakachozalishwa kikajaza soko la Saudi Arabia" Amesema Mwadini
Amesema kuwa nchi hiyo inaagiza bidhaa kutoka nje za nchi kwani inawakazi zaidi ya milioni 35 na wanazalisha chakula chao kwa asilimia tano na asilimia 95 wanaagiza kutoka nchi nyingine.
Pia Mwadini amesema Tanzania imepata kibali cha kusafirisha Nyama pamoja na Mifugo hai kuipeleka Nchi ya Saudi Arabia kwaajili ya kukuza uchumi.
Amesema wawekezaji wa nchi hiyo wamekuja nchini kukamilisha taratibu za uwekezaji na kukuza mahusiano ya kiuchumi baina ya Tanzania na Saudi Arabia
Balozi wa Tanzania Nchini Saudi Arabia, Ali Mwadini akizungumza katika Kikao na wawekezaji kutoka nchini Saudi Arabiakilichofanyika leo Agosti 11,2022 katika ofisi za TIC jijini Dar Es SalaamBalozi wa Tanzania Nchini Saudi Arabia, Ali Mwadini akiwa katika Kikao na wawekezaji kutoka nchini Saudi Arabiakilichofanyika leo Agosti 11,2022 katika ofisi za TIC jijini Dar Es Salaam
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Revocatus Rasheli akizungumza katika Kikao na wawekezaji kutoka nchini Saudi Arabiakilichofanyika leo Agosti 11,2022 katika ofisi za TIC jijini Dar Es Salaam.
Social Plugin