Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC MJEMA AAGIZA MAKARANI WALIOMALIZA KAZI KWENYE MAENEO YAO WAHAMISHIWE MAENEO YALIYOSALIA


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema leo Jumapili Agosti amefanya ziara ya kukagua mwenendo wa zoezi la uandikishaji Sensa ya watu na makazi kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.

Mhe. Mjema ametembelea maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la Mgodi Mwime Kata ya Zongomela.

Akiwa katika Maeneo hayo Mhe. Mjema amewaagiza Viongozi katika kila wilaya na waratibu wa sensa katika mkoa wa Shinyanga kuchukua hatua ya haraka kwa kuwahamisha makarani wa sensa waliokamilisha kazi kwenda katika maeneo mengine yaliyosalia ili kuongeza nguvu na kasi ya kuhesabu kaya na makazi.

Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Ndg. Clemence Mkusa amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa hakuna atakayeachwa kuhesabiwa kwani mwenendo wa uandikishaji unaenda vizuri.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com