Shaka akinyooshea kidole picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akimwelezea juu ya kasi ya utekelezeji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Kijiji cha Uliyankulu, Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora.
******
*Asema CCM inaridhishwa na jitihada zake za kuwaleta maendeleo wa Watanzania
*Aanika ujenzi hospitali za wilaya zilizojengwa ndani ya mwaka mmoja
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye suala la maendeleo ni kama Kulwa na Doto.
Ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wananchi wa maeneo mbalimnali wa wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambapo pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo kueleza CCM inampongeza Rais Samia kwa jitihada anazofanya za kupeleka maendeleo kwa wananchi wakiwemo wa Kaliua na Mkoa wa Tabora kwa ujumla.
“Hapa Kaliua Rais Samia amefanikisha ujenzi wa hospitali na kwa mujibu wa taarifa zilizopo ilikwama kwa miaka 10 kutoka mwaka 2012 mpaka 2022 lakini Rais Samia amekuja kukwamua mkwamo huu ili wananchi mpate huduma.Narudia tena kueleza Rais Samia kwenye maendeleo ni kama Kurwa na Doto ,niliwaambia Rais Samia halali, hatulii, hali vizuri na yote ni kwa ajili ya kuhakikisha wananchi watanzania wananufaika na fursa za kimaendeleo.
“Sasa Rais amefanya jambo kubwa sana kwa kuja kukwamo huo ambao umekwama kwa zaidi ya miaka 10, hospitali hii ilikwama ndani ya mwaka mmoja ujenzi kwa kuimalizia hii kazi na ndio maana nasema kama katika maendeleo ni Kurwa na Doto, amefanya kazi kubwa kwenye sekta ya afya,
“Rais Samia ukienda kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi tumeahidi mpaka ikifika mwaka 2025 tutakuwa tumejenga hospitali za halmashauri 98 kwa taarifa yenu niwaambie mpaka ninavyozungumza ameshajenga hospitali za halmashauri za wilaya 58 , ndani ya mwaka mmoja na miezi mitano.
“Ndio maana tunasema ni kulwa na doto , lakini hayo anayofanya hayafanyi kwa utashi wake bali amefanya kwasababu ni maelekezo ya Ilani ya uchaguzi ya CCM.Ukienda kusoma Ibara ya 83 kifungu F kinaeleza hayo ambayo nimeyasema kwamba katika kipindi cha miaka mitano Serikali ya CCM itajenga hospitali 98 za halmashauri ya wilaya.
“Ndani ya mwaka mmoja na miezi mitano Rais Samia ametoa fedha na hospitali hizo 58 ujenzi umeanza kwenye mwaka wake wa kwanza wa bajeti ya serikali na hospital 31 ujenzi unaendelea.Zimetimia hospitali 58 lakini Rais Samia hakuishia hapo hata hii hospitali yenu itapata vifaa tiba,”amesema Shaka.
Ameongeza Rais Samia ameandika historia kwenye nchi hii na anakuwa Rais wa kwanza ambaye anatoa fedha za mejengo na fedha za vifaa.“Rais katika kipindi chake cha mwaka mmoja ametoa bilioni 47 kwa ajili ya vifaa tiba katika hospitali 159 katika nchi hii lakini katika kipindi chake cha mwaka wa 2022/2023 anakwenda kujenga vituo 300 vya afya.
“Kwenye hii haijapata kutokea, Rais Samia ametenga zaidi ya Sh.bilioni saba kwa ajili ya vifaa tiba vya masikio na macho. Vipi utasema sio kurwa na doto? Rais Samia ametenga Sh.bilioni 17 kwa ajili ya hospitali hizo 300 ambazo zinakwenda kujengwa kwenye nchi hii,”amesema.
Ameongeza huko nyuma tulikotoka walikuwa wanajenga majengo mengi sana lakini yalikuwa yabakia kuwa masalia ya ndege kwani yalikuwa yanakamilika lakini vifaa hakuna yanafungwa yanachukua miaka miwili au miaka mitatu.
Amesema Rais Samia amefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya , anajenga wakati huo huo anatoa fedha kwa ajili ya vifaa tiba.”Rais Samia, Mbunge na madiwani hawataangusha kwenye uongozi wao kwani hawa ni mapacha watatu na wanayoyafanya ni kwa maslahi mapana ya wananchi wa jimbo hilo na majimbo mengine.
“Chama Cha Mapinduzi hii ndiyo kazi yetu tumekuja kufuatilia, tumekuja kuona ,tumekuja kujiridhisha ambavyo Ilani inatekelezwa lakini tumekuja tuwasikilize wananchi na ndio maana tunapoona mambo hayaendi vizuri tunasema mambo hayaendi.
“Nyie Tabora mna bahati sana,nataka niwaambie miradi mikubwa ya maendeleo inaletwa kwenye mkoa, huu , hospitali maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu inaletwa mkoa huu, Rais samia kwenye bajeti ya mwaka huu ametenga Sh.bilioni 120 na atazimwaga mkoa wa Tabora.Mambo anayofanya Rais Samia kwenye wilaya hii ya Kaliua ni mengi.”
Shaka akizungumza na Wana CCM na wananchi katika Shina Namba 5, Kijiji cha Uliyankulu, Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ( ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, (katikati) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Tabora kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 mkoani humo, kushoto ni mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Batilda Burian na kulia ni Solomon Kasaba. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, (katikati) akizungumza na wananchi katika kijiwe cha kahawa Lumumba, mjini Tabora.
Shaka na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Gilbert Kalima, wakishiriki ujenzi wa kituo cha Afya Mwongozo kilichopo Kata ya Mwo,ngozo, wilayani Kaliua Mkoa wa Tabora.