*********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Klabu ya Simba imefanikiwa kuondoka na alama tatu mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi Kuu NBC, mchezo ambao ulichezwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam
Simba Sc imeweza kupata mabao 2-0 ambayo yalifungwa na mastaa wao Moses Phiri pamoja na mshambuliaji wao Dejan Georgjevic.
Mpaka Mapumziko Simba Sc ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 ambalo lilifungwa baada ya Okrah kupiga mpira wa adhabu ambao ulimshinda goli kipa Kipao na Moses kufunga.
Social Plugin