****************
NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Simba ikiwa inajindaa kwa michezo ya ligi inayofuata, leo hii imeshuka dimbani kumenyana na Asante Kotoko nchini Sudan.
Asante Kotoko ndiyo walianza kupata bao katika dakika ya 9 ya mchezo kabla ya kiungo mshambuliaji wa Simba Sc Augustine Okrah kufunga bao zuri la kusawazisha kwenye mchezo huo.
Simba iliendelea kucheza soka safi la kushambulia na kumiliki mpira na baadae kupata mabao mengine ya haraka kabla ya mapumziko na matokeo kuwa 3-1, mabao ambayo yalifungwa na pia na Clautos Chama pamoja Pape Sakho.
Bao lingine ambalo lilifanya ubao usomeke 4-1 lilifungwa tena na Clautos Chama . Simba itaendelea kucheza mechi za kirafiki kwa kipindi hiki ligi ya NBC ikiwa imesimama kwa muda kupisha mashindano ya kuwania kufuzu CHAN mwakani.
Social Plugin