MENEJA wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Ziwa Mhandisi Joseph Mwaipaja, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda la TBS wakati wa Maonesho ya Nanenane yenye kauli mbiu 'Kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Uvuvi na Mifugo''yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyamhongolo wilayani Ilemela jijini Mwanza.
MENEJA wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Ziwa Mhandisi Joseph Mwaipaja,akiwahimiza wananchi kufika kwenye banda lao ili kupata elimu zaidi juu ya bidhaa wakati wa Maonesho ya Nanenane yenye kauli mbiu 'Kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Uvuvi na Mifugo''yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyamhongolo wilayani Ilemela jijini Mwanza.
Afisa mdhibiti ubora kutoka TBS Bw.Arnold Kubingwa,akitoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kudhibitisha bidhaa zao wakati wa Maonesho ya Nanenane yenye kauli mbiu 'Kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Uvuvi na Mifugo''yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyamhongolo wilayani Ilemela jijini Mwanza.
Charles Safari Mkazi wa Igoma Bw.Charles Safari akimuuliza swali Afisa mdhibiti ubora wa TBS Bw.Arnold Kubingwa mara baada ya kupata elimu katika banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane yenye kauli mbiu 'Kilimo ni biashara,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,Uvuvi na Mifugo''yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyamhongolo wilayani Ilemela jijini Mwanza.
..........................................
Na Hellen Mtereko-MWANZA
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linaendelea kutoa elimu kwa Wananchi na wafanyabiashara katika maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyamhongolo Wilayani Ilemela jijini Mwanza.
Akizungumza kwenye banda la TBS Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa Mhandisi Joseph Mwaipaja, amesema lengo la kuendelea kutoa elimu ni kuwasaidia wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kufahamu umuhimu wa kudhibitisha bidhaa zao.
Amesema TBS inafanya udhibiti wa bidhaa zote sokoni zinazoingia na zinazozalishwa ndani ili kuweza kuwasaidia watanzania kupata bidhaa ambazo ni salama na zinazokidhi ubora kwa matumizi ya binadamu.
"Tunaendelea kutoa elimu kwa Wananchi wote wa Kanda ya ziwa ili waweze kujua ni hatua gani ambazo zinatakiwa kufuatwa kwa ajili ya kupata nembo ya ubora itakayowasaidia kuuza bidhaa zao kwa usalama",amesema Mhandisi Mwaipaja
Mhandisi Mwaipaja amesema kutokana na kauli mbiu ya mwaka huu isemayo "Ajenda 1030 kilimo ni biashara shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo, mifugo na uvuvi inabidi watanzania wawe na utaratibu wa kudhibitisha ubora wa bidhaa ili wawe na uzalishaji ambao ni endelevu katika mnyororo wa thamani.
Ameeleza kuwa Mkoa wa Mwanza ni Mji wa kimkakati hivyo wafanyabiashara wakifuata taratibu zote za kupata nembo ya ubora kutoka TBS watakuwa na uwezo wa kuuza bidhaa zao bila kukaguliwa na Nchi uanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mwaipaja amesema TBS kupitia Serikali inautaratibu wa kutoa nembo bure kwa wajasiriamali wote waliopitia kwenye taasisi ya Sido wanaotengeneza bidhaa.
Social Plugin