Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi kama ifuatavyo:
1) Amemteua Balozi Mwanaidi Sinare Maajar kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Balozi Maajar anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji mstaafu, Mhe. Damian Lubuva ambaye alimaliza muda wake.
2) Amemteua Prof. William Andey Lazaro Anangisye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA). Prof. Anangisye anaendelea kwa kipindi cha pili.
Uteuzi huu unaanza tarehe 23 Agosti, 2022.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Social Plugin