Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI DKT MABULA ASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI KUU YA SENSA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula (Kulia) na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama (Wa pili kushoto) wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Mchemba wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya Sensa kilichofanyika Agosti 18, 22 jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula (Kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya Sensa kilichofanyika Agosti 18, 2022 jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wa Kikao cha Kamati Kuu ya Sensa kilichofanyika Agosti 18, 2022. ( PICHA NA WIZARA YA ARDHI)


********************

AGOSTI 18, 2022 DAR ES SALAAM

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameshiriki kikao cha Kamati Kuu ya Sensa kwa ajili ya kupokea taarifa ya Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi inayotarajia kufanyika kuanzia Agosti 23, 2022.

Kikao hicho kilichoongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kimefanyika tarehe 18 Agosti 2022 katika ukumbi wa kituo cha Mwl Nyerere Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa pili wa rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah pamoja na Mawaziri wa serikali ya Muungano na Mapinduzi.

Katika kikao hicho Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliwaeleza wajumbe wa Kikao hicho kuwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia tarehe 23 Agosti 2022 iwe siku ya mapumziko.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com