WAZIRI MBARAWA ATEMBELEA MRADI WA BRT II, AFURAHISHWA NA KASI YA UJENZI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akimuelekeza jambo Msimamizi wa Mradi wa BRT II, Mhandisi Bw.Frank Mbilinyi mara baada ya kutembelea mradi wa BRT II leo Agosti 17,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akiwa pamoja na wahandisi wa ujenzi akitembelea mradi wa BRT II leo Agosti 17,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mradi wa BRT II leo Agosti 17,2022 Jijini Dar es Salaam.Msimamizi wa Mradi wa BRT II, Mhandisi Bw.Frank Mbilinyi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa kutembelea mradi wa BRT II leo Agosti 17,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akizungumza na wanaohusika na ujenzi wa mradi wa BRT II Mbagara mara baada ya kutembelea mradi wa huo leo Agosti 17,2022 Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa daraja bandari kwaajili ya kutumika mradi wa BRT II

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi BRT II umefikia asilimia 66.6 na unategemewa ujenzi huo kukamilika ifikapo Mwezi Februari, 2023.

Ameyasema hayo leo Agosti 17,2023 mara baada ya kutembelea ujenzi wa mradi huo ambapo amesema hali inaenda vizuri kwa ujumla na kuna mategemeo kumalika kwa muda ambao umewekwa ili mradi huo uweze kufanya kazi.

"Miundombinu muhimu ambayo inatakiwa kusimamiwa kwa makini ni miundombinu ya madaraja hivyo katika daraja lililopo bandarini tumekubaliana kufikia mwezi Desemba 2022 liwe limekamilika na madaraja mengine kufikia Mwezi Januari, 2023 yawe yamekamilika". Amesema Waziri Mbarawa.

Aidha Waziri Mbarawa amewataka wahandisi wanaosimamia ujenzi wa mradi huo kuhakikisha wanaendelea kujenga barabara hiyo na kusimamia kwa viwango walivyokubaliana kwenye mkataba na mpaka sasa kazi ni nzuri na wao waendelee kusimamia.

Pamoja na hayo amewataka wale ambao wapo karibu na mradi waendelee kutoa ushirikiano kwa mkandarasi ili mradi huo umalizike mapema iwezekanavyo ili tuweze kuona matokeo yake kwa muda mfupi.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi wa BRT II, Mhandisi Bw.Frank Mbilinyi amesema kuwa wanatarajia daraja lililopo bandarini kumalizika na magari kuanza kupita kufikia Mwezi Oktoba mwishoni wakati madaraja mengine yameshakamilika kwa upande mmoja na magari yameruhusiwa kupita.

"Madaraja kama pale Chang'ombe, upande mmoja umeshafunguliwa na upande mwingine unaendelea kujengwa na ile fly over ya pale Mandela na Kilwa Road imeshamalizika upande mmoja na magari yanapita na upande mwingine unaendelea kujengwa, ni matazmio yetu makubwa hata hili la bandarini linaweza kukamilika kwa kipindi kizuri". Amesema Mhandisi Mbilinyi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post