Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Ummy Nderiananga.
Na Dotto Kwilasa, DODOMA
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma Ummy amesema vifaa hivyo vitawezesha Ofisi ya waziri mkuu kutekeleza shughuli za uratibu na udhibiti wa maafa mbalimbali hasa katika kuchukua taarifa katika picha ili kupata majanga na madhara pindi yanapotokea katika nyanja za sekta na taasisi za serikali.
Ameeleza kwamba vifaa hivyo ni muhimu kwa kuzingatia jukumu kuu la Ofisi ya Waziri Mkuu ambalo ni Uratibu wa shughuli za Serikali na uratibu wa shughuli za maafa na taasisi zisizo za kiserikali kwa njia ya mtandao.
“Kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, tunaishukuru WFP binafsi na shirika la WFP kwa kutupatia vifaa hivi muhimu kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano kwa njia ya mtandao, kufanya operesheni za utafutaji na uokoaji, kupata ramani za hatari zilizopo, uwezekano wa kuathiriwa na janga na uwezo wa jamii husika,”amesema Naibu waziri huyo.
Aidha ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ambayo yamekuwa yakiiunga mkono Serikali katika miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi na Taifa.
Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Ummy Nderiananga, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. John Jingu amebainisha kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu iko tayari kushirikiana na (WFP) kwa kila eneo ambalo watahitaji ushirikiano huku akiahidi vifaa hivyo kutumika kama ilivyokusudiwa.
“Tunakumbana na maafa mengi na huwa inachukua mda mrefu kwa waokozi au upataji wa taarifa unachelewa hivyo,kwaajili ya hizi drone naamini ufanyaji kazi na upatikanaji wa uhalisia wa tukio utapatikana kwa urahisi”amesema
Aidha Mkurugenzi Mkazi Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)Sarah Gibson mefafanua kuwa mradi huo ni endelevu kwa miaka mitano kuanzia Julai 2022 hadi Juni 2027 na kwamba Shirika litafanya kazi zake kulingana na vipaumbele vya serikali na kuwenkeza katika kilimo, elimu na maafa
Social Plugin