Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulyutu akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea mafanikio ya Sekta ya Afya awamu ya Sita.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulyutu akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea mafanikio ya Sekta ya Afya awamu ya Sita.
Na Halima Khoya - Shinyanga
Licha ya kuwepo kwa changamoto za kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi nchini Mkoa wa Shinyanga umefanikiwa kujenga Hospitali ya Rufaa Mkoa Shinyanga , Zahanati na vituo vya afya kwa mwaka wa fedha 2022/23 ikiwa ni njia ya kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.
Akizungumza na Waandishi wa habari Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulyutu ambaye ni Mratibu wa miundombinu ya afya Mkoa wa Shinyanga amesema katika kuboresha huduma za afya mkoani Shinyanga wamefanikiwa kujenga Hospitali mpya ya Rufaa iliyopo Mwawaza Manispaa ya Shinyanga ambayo tayari imeanza kutoa huduma za afya.
“Katika mikakati ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan serikali ya mkoa huu imejenga hospitali ya Rufaa ya Mkoa iliyopo Mwawaza ambapo hospitali ya Mkoa Shinyanga itakuwa hospitali ya Manispaa ya Shinyanga ili kwa wagonjwa watakaoshindikana kutibiwa katika hospitali ya manispaa wapelekwe katika hospitali ya Mkoa Mwawaza", amesema Mulyutu.
“Katika awamu hii ya sita tumepata fedha nyingi na kujenga miundombinu ya Hospitali na zahanati kila Halmashauri. Tumefanikiwa pia tumefanikiwa kujenga majengo mengi yakiwemo ya huduma ya dharura, Mlipuko wa Magonjwa, Wagonjwa Mahututi, na jengo la kuzalisha hewa ya Oksijeni, hali itakayopelekea kurahisisha upatikanaji huduma za afya kwa wananchi",amesema.
Katika hatua nyingine amesema miongoni mwa mikakati ya serikali ni kujenga vituo vya afya kwenye kila kata na vijiji katika Mkoa hali itakayosaidia wananchi kupatiwa huduma za afya kwa haraka katika jamii.
“Katika mikakati hiyo serikali haijawaacha mbali wananchi wanaoishi vijijini, tumejenga baadhi ya majengo ya vituo vya afya katika maeneo hayo ili kuondokana na kilio cha wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya”, ameongeza Mulyutu.
Social Plugin