Kamishna wa Tume ya Madini ,Janeth Lekashingo (katikati) akifunga warsha ya ya ushirikishwaji wananchi katika mnyororo wa sekta ya madini (Local Content iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu mwishoni mwa wiki (Kushoto) ni Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Jan Jacobs (kulia) ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Madini kutoka tume hiyo,Bw.Venance Kasiki.
Meneja wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa, akitoa mada wakati wa semina ya ushirikishwaji wananchi katika mnyororo wa sekta ya madini (Local Content iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu mwishoni mwa wiki,(Kulia) ni Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Jan Jacobs.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa semina hiyo
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa semina hiyo
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa semina hiyo
Washiriki katika picha ya pamoja na Kamishna wa Tume ya Madini
***
Kamishna wa Tume ya Madini nchini, Janeth Lekashingo, ameipongeza kampuni ya madini ya Barrick kwa jitihada inazofanya kuhakikisha inatekeleza sera ya ushirikishwaji wananchi katika mnyororo wa sekta ya madini (Local Content) kwa lengo la kuwanufaisha Watanzania wanaoishi jirani na migodi yake.
Akifunga semina ya siku mbili iliyohusu ushirikishwaji wananchi katika mnyororo wa sekta ya madini (Local Content) iliyoandaliwa na Twiga Minerals Corporation na kufanyika katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, Bi. Lekashingo, alisema Barrick ni miongoni mwa makampuni ambayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza sera hii kwa vitendo.
Semina hiyo ilihusisha wafanyakazi wa Barrick na Maofisa kutoka Tume ya Madini ambao walitoa mada mbalimbali kuhusiana na uendeshaji wa shughuli za uchimbaji madini nchini kwa kufuata sheria na miongozo ya Serikali.
"Nawapongeza sana kwa kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza sera hii kwa vitendo na pia kufanikisha miradi ya maendeleo katika maeneo yanayozunguka migodi yenu kupitia fedha za uwajibikaji katika jamii (CSR)", alisema Lekashingo.
Alisema moja ya majukumu ya Tume ya Madini ni kusimamia wadau katika sekta ya madini kuhakikisha wanatekeleza sera hii hususani katika utoaji wa zabuni kwa makampuni ya wazawa yaliyosajiliwa na tume hiyo na makampuni ya nje yanayoshirikiana na wazawa ikiwemo suala la kutoa ajira kwa wazawa.
Aliongeza kusema Tume ya Madini iko tayari kutoa ushauri wa kitaalamu bure kwa Barrick na wadau wengine katika sekta ya madini kuhakikisha sera hii inatekelezwa na kufanikisha lengo lake la kuwawezesha watanzania kunufaika na sekta ya madini.
Akiwasilisha mada ya utendaji wa shughuli za Barrick, Meneja wake nchini Georgia Mutagahywa, alisema hadi kufikia sasa takribani asilimia 70% ya watoa huduma katika migodi ya Barrick nchini ni Watanzania.
“Kampuni imefanikiwa kutekeleza sera hii kwa vitendo katika maeneo ya ajira, utoaji wa zabuni, sambamba na kuendesha miradi ya kusaidia jamii katika maeneo yanazozunguka migodi yake nchini kupitia fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuhudumia jamii (CSR)” ,alisema Mutagahywa.
Aliongeza kuwa Barrick, tayari imeanzisha programu ya kuwaendeleza wafanyabiashara wa ndani,(Local Business Development Programme (LBD) inayosimamiwa na mgodi wa North Mara, ambayo ni mhimili wa kusimamia kanuni hii na kuhakikisha watanzania wananufaika nayo kwa asilimia kubwa kwa kuboresha maisha yao kupitia uwekezaji katika sekta ya madini, na fursa zilizopo kwenye sekta hii na tayari baadhi ya wafanyabiashara wamepatiwa mafunzo katika awamu ya kwanza.
Watendaji kutoka Tume ya Madini pia walipata fursa ya kutembelea mgodi wa Bulyanhulu na kujionea shughuli za uchimbaji zinazofanywa na Barrick kwa kutumia teknolojia za kisasa zenye viwango vya kimataifa vilevile walitembelea kituo cha afya za Bugarama wilayani Msalala ambacho kimeboreshwa na kuwa cha kisasa kupitia fedha za Uwajibikaji wa jamii zilizotolewa na kampuni hiyo.
Serikali ya Tanzania iliunda sera ya Local content mwaka 2017 ikilenga sekta ya madini, mafuta na gesi ili kuhakikisha uchimbaji wa madini na mapato yake yanawanufaisha watanzania.
Sera hiyo na kanuni zake inalenga kupanua uwanda wa kibiashara kwenye uchumi wa Tanzania, kutengeneza nafasi za ajira kwa kuhamasisha maendeleo ya taaluma na uwezo wa watanzania kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi nchini.
Social Plugin