Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BIBI WA MIAKA 70 ATANGAZA KUWA NI BIKRA...SASA ANATAFUTA MCHUMBA AOLEWE


Alphonsine Tawara mwenye umri wa miaka 70, amefichua kuwa bado ni mwanamwali na bikira.

Mwanamke huyo raia wa Congo, alieleza kuwa alijitolea maisha yake yote kuwalea ndugu zake na sasa yuko tayari kuolewa iwapo atapata mwanaume.

Akizungumza katika mahojiano na AfriMax, alisema: 

"Sababu ya mimi bado kuolewa ni kwa sababu sijapata mwanaume anayenifaa. Lakini nilipokuwa bado msichana mdogo, wanaume kadhaa walikuwa wakinifuata. Nilichumbiana na watu kadhaa lakini nilikataa kuolewa kabla ya ndugu zangu kuhitimu kwa sababu Mimi ndiye nilikuwa nikiwatunza."

Alphonsine alisema alisubiri hadi wadogo wake walipohitimu chuo kikuu lakini hakupata bahati ya kuolewa. 

"Wanaume walikuwa wanataka kunioa lakini nilikuwa nikiwaambia hapana kwa sababu nilitaka kuwasomesha ndugu zangu kwanza, kisha kuolewa baadaye," alisimulia. Mwanamke huyo alitumikia maisha yake yote kuwasomesha jamaa zake hadi alipozeeka.

Alphonsine, ambaye ni mwalimu kitaaluma, anafunza mara nyingi katika shule za Kikatoliki. "Sina mtoto wangu binafsi lakini mimi ni mama wa wengi - watoto ambao nimewafundisha." "Nikipata mume, nitaolewa. Niko tayari kuwa mke na kuhama kuishi pamoja na mume wangu," alisema.

 Alphonsine anasema alikuwa makini asiishie kuwa mama msimbe na mara nyingi alikuwa akiwafukuza wanaume. Mwalimu huyo aliwashauri wasichana kuhifadhi ubikra wao kabla ya ndoa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com