Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KIFO CHA QUEEN ELIZABETH II


Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na kifo cha Malikia Elizaberth II wa nchini Uingereza, kilichotokea jana Alhamisi Septemba 8, 2022 katika visiwa vya Balmoral nchini Scotland alipokuwa anapatiwa matibabu.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia ameandika, “Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Malkia Elizabeth II. Kwa niaba ya Watanzania wote, natuma salamu za pole kwa familia ya Kifalme@RoyalFamily na raia wote wa Uingereza. Malkia atakumbukwa duniani kote kama nguzo ya Amani, Umoja na Utulivu.”
Elizaberth II alizaliwa jijini London April 21, 1926, aliukwaa wadhifa wa Malkia akiwa na umri wa miaka 25, mnamo mwaka 1952 baada cha kifo cha baba yake aliyekuwa mfalme wa taifa wa taifa hilo David IV.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com