Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye ameiwakilisha Tanzania kwenye uchaguzi wa Katibu Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) pamoja na Naibu wake, uliofanyika tarehe 29 Septemba, 2022 jijini Bucharest, Romania, kwenye Mkutano Mkuu wa ITU Plenipotentiary 2022 (ITU PP22).
Viongozi wanaochaguliwa kwenye Mkutano huo wataiongoza ITU kwa kipindi cha Miaka Minne kuanzia 2024 - 2027.
Waziri Nape mara baada ya uchaguzi huo, atatoa tamko la Kisera la Tanzania kwa wajumbe wa ITU PP22.
Social Plugin