DC MBONEKO NA DK. MBONEKO WAGAWA 'SUNSCREEN LOTION' KULINDA NGOZI ZA WATOTO WENYE UALBINO SHINYANGA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye kituo cha watoto wenye uhitaji maalum Manispaa ya Shinyanga, alipofika kugawa Lotion kwa ajili ya kulinda ngozi kwa watoto wenye Ualbino.

Muonekao wa Lotion zikiwa ndani ya boksi ambazo wamepewa watoto wenye Ualbino kwa ajili ya kulinda ngozi zao.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akigawa Lotion kwa watoto wenye Ualbino akiwa na Dk. Mike Mboneko.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amegawa Lotion kwa watoto wenye Ualbino ambao wanalelewa kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kulinda afya ya ngozi zao.

Mboneko amegawa Lotion hizo leo Septemba 21, 2022 akiwa ameambatana na Maofisa elimu Maalum, pamoja na Madaktari.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa Lotion hizo, amesema Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuwahudumia watoto wenye ulemavu kwa kuwawekea mazingira rafiki ya kusoma, pamoja na kuwapatia lotion kwa ajili ya kulinda afya ya ngozi zao.

“Tunawashukuru Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga, pamoja na Mkurugenzi kwa kutoa fedha Sh.milioni 5.8 na kununua Lotion hizi tube 300 na leo tunawapatia watoto hawa wenye Ualbino ili kulinda ngozi zao,”amesema Mboneko.

“Tunaomba wadau mbalimbali waendelee kujitokea kusaidia watoto hawa wenye uhitaji kama alivyokuwa akifanya Hayati Dk. Reginald Mengi na kuwapunguzia baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili ili wasome kwa furaha na kutimiza ndoto zao,”ameongeza.

Aidha, amewataka Madaktari wawe wanatembelea mara kwa mara kwenye kituo hicho cha watoto wenye Ualbino na kuangalia afya zao.

Naye Mtoto Wande Juma, akizungumza kwa niaba ya wenzake ameshukuru kupewa msaada huo wa Lotion ambazo zitawasaidia kulinda ngozi zao.

Naye Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dk, Elisha Robert, amesema Manispaa hiyo ya Shinyanga imenunua Lotion tube 300 zenye jumla ya thamani ya Sh.milioni 5.8 na katika kituo hicho cha Buhangija kuna jumla ya watoto wenye Ualbino 110 ambao watapewa tube mbili mbili.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye kituo cha watoto wenye uhitaji maalum Manispaa ya Shinyanga, alipofika kugawa Lotion kwa ajili ya kulinda ngozi kwa watoto wenye Ualbino.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Buhangija Jumuishi Fatuma Jilala ambaye ndiye mlezi mkuu wa kituo hicho, akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ya kugawa Lotion kwa watoto wenye Ualbino.

Mtoto mwenye Ualbino Wande Juma akitoa neneo la shukrani kwa niaba ya wenzake mara baada ya kumaliza kupewa Lotion kwa ajili ya kulinda ngozi zao.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akigawa Lotion kwa watoto wenye Ualbino kwa ajili ya kulinda afya ya ngozi zao.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akigawa Lotion kwa watoto wenye Ualbino kwa ajili ya kulinda afya ya ngozi zao.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiangalia Ngozi ya Mtoto mwenye Ualbino alipofika kugawa Lotion kwa ajili ya kulinda ngozi zao.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipiga picha ya pamoja na watoto wenye Ualbino huku wakiwa wameshikilia Lotion walizopewa kwa ajili ya kulinda Ngozi zao.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kushoto) akimpatia pesa Mwalimu Fatuma Jilala kwa ajili ya chakula cha watoto hao wenye mahitaji maalumu, (katikati) Dk, Mike Mboneko, (kushoto) Dk. Elisha Robert.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dk. Elisha Robert akigawa Lotion kwa watoto wenye Ualbino kwa ajili ya kulinda ngozi zao.

Dk. Mike Mboneko akigawa Lotion kwa watoto wenye Ualbino kwa ajili ya kulinda ngozi zao.

Muonekao wa Lotion zikiwa ndani ya boksi ambazo wamepewa watoto wenye Ualbino kwa ajili ya kulinda ngozi zao.

Watoto wenye Ualbino wakiwa wameshika Lotion ambao watazitumia kwa ajili ya kulinda ngozi zao.

Dk. Mike Mboneko akipiga picha ya pamoja na watoto wenye Ualbino huku wakiwa wameshika Lotion kwa ajili ya kulinda ngozi zao.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kugawa Lotion kwa watoto wenye Ualbino.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post