Mwaka 2022, Marekani inatawala katika orodha ya miji 20 tajiri zaidi ulimwenguni ambapo na majiji sita ya Marekani yameingia katika orodha hiyo. Miji miwili ya Uswizi pia imeingia kwenye 20 bora, pamoja na miji nane ya ukanda wa Asia-Pacific kwa mujibu wa ripoti kutoka New World Wealth na Henley & Partners.
New York - jiji tajiri zaidi duniani
Times Square, New York
New York au Big Apple ni makazi ya mamilionea 345,600, wakiwemo mamilionea 737 (wenye utajiri wa dola milioni 100 au zaidi) na mabilionea 59 wa dola.
New York ndio kitovu cha fedha kwa USA na jiji tajiri zaidi ulimwenguni kwa vipimo kadhaa.
Pia ni eneo lenye ubadilishanaji mkubwa zaidi wa hisa ulimwenguni kwa kiwango cha soko (Dow Jones na NASDAQ). Labda haswa zaidi, jumla ya utajiri binafsi unaoshikiliwa na wakaazi wa jiji hilo unazidi dola za Marekani trilioni 3 kiasi ambacho ni cha juu kuliko jumla ya utajiri binafsi unaoshikiliwa katika nchi nyingi kuu za G20.
Jiji hilo linajumuisha halmashauri tano za Bronx, Brooklyn, Manhattan, Queens, na Staten Island na inashirikisha baadhi ya mitaa ya tajiri zaidi ulimwenguni, ikiwemo 5th Avenue huko Manhattan ambapo bei za nyumba za kupanga zinaweza kuzidi dola ya Marekani 28,000 kwa kila mita ya mraba.
Ikumbukwe kwamba kuna miji kadhaa ya watu matajiri iliyo nje kidogo ya Jiji la New York ambayo pia ina kiasi kikubwa cha utajiri wa ngazi ya juu. Maarufu ni pamoja na: Greenwich, Great Neck, Sands Point na Old Westbury.
Ikiwa miji hii ingejumuishwa katika takwimu za Jiji la New York, basi idadi ya mabilionea katika jiji iliyojumuishwa ingezidi 120.
Tokyo - mji mkuu wa Japan katika nafasi ya 2
Tokyo ina wakazi mamilionea 304,900, wakiwemo mamilionea 263 na mabilionea 12.
Idadi yake ya chini ya mabilionea ikilinganishwa na miji mingine mingi kwenye orodha ya 20 bora inaonyesha kuwa utajiri unagawanywa kwa usawa huko Tokyo, huku watu wa tabaka la kati na mamilionea wa chini wakidhibiti utajiri mwingi wa jiji.
Kampuni kuu zilizoko Tokyo ni pamoja na Honda, Hitachi, Mitsubishi, Softbank, na Sony.
Eneo la San Francisco Bay - linakuja kwa kasi
Eneo la San Francisco Bay - linalojumuisha jiji la San Francisco na Silicon Valley ni makazi ya mamilionea 276,400, wakiwemo mamilionea 623 na mabilionea 62.
Makazi yenye idadi kubwa ya mabilionea wa teknolojia, Silicon Valley inajumuisha miji tajiri kama vile Atherton na Los Altos Hills.
Eneo hili limekuwa likipanda kwa kasi katika orodha ya vitovu vya mamilionea katika muongo mmoja uliopita na linatarajia kufikia kileleni ifikapo 2040.
London - bado ni kivutio cha milionea wa juu
Mji tajiri zaidi duniani kwa miaka mingi, leo hii mamilionea 272,400 wanaita London nyumbani kwao, idadi ambayo inajumuisha mamilionea 406 na mabilionea 38.
Nyumba na vyumba vya kupanga ambapo bustani za kuvutia London kama vile Hyde Park na Regents Park, na maeneo ya kijani kibichi kama vile Hampstead Heath ni tajiri sana. Vitongoji tajiri zaidi vya London vinaonyeshwa katika ramani inayotolewa na wataalamu wa uchanganuzi wa eneo Webster Pacific.
Ikumbukwe kwamba London imekuwa na mtiririko wa kutosha wa mamilionea katika muongo mmoja uliopita huku wengi wakiondoka jiji hilo kwenda katika miji ya pembeni kama vile Ascot, Beaconsfield, Bourne End, Bray, Cookham, Henley, Leatherhead, Maidenhead, Marlow, Taplow, Virginia Water, Weybridge, na Windsor.
Kuna sababu kadhaa zinazosababisha kuhama ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa viwango vya uhalifu katika jiji.
Singapore - Jiji la kibiashara
Linashika nafasi ya 5 duniani, Singapore ni eneo la pili kwa ukubwa la mamilionea barani Asia baada ya Tokyo.
Ni makazi kwa mamilionea 249,800, wakiwemo mamilionea 336 na mabilionea 26, jiji hilo linachukuliwa kuwa jiji linalofaa zaidi kibiashara na ni mojawapo ya eneo lenye mamilionea wahamiaji wengi.
Watu binafsi takriban 2,800 wenye utajiri wa juu wanatarajiwa kuingia kwa mwaka wa 2022 pekee kwa mujibu wa taarifa ya Henley Private Wealth Migration.
Los Angeles - kitovu cha burudani duniani
Eneo hili ni nyumbani kwa mamilionea wakazi 192,400, ikiwa na mamilionea 393 na mabilionea 34. Takwimu za eneo hili zinajumuisha utajiri unaoshikiliwa katika jiji la Los Angeles, pamoja na Malibu iliyo karibu, Beverly Hills, Laguna Beach, Newport Beach, na Santa Monica.
Sekta kuu ni pamoja na burudani, IT na usafirishaji.
Chicago - uchumi wa aina mbalimbali
Jiji kubwa zaidi la bara nchini Marekani na nyumbani kwa mamilionea 160,100, ikiwa ni pamoja na mamilionea 340 na mabilionea 28, Chicago, ina uchumi wa aina mbalimbali ambao una nguvu katika sekta nyingi muhimu. Chicago ndio mji msingi kwa kampuni 35 katika orodha ya makampuni makubwa 500 ya jarida la Fortune kama vile kama vile McDonalds na Boeing.
Houston - moja ya miji inayokua kwa kasi zaidi ulimwenguni
Jiji la Houston lina mamilionea 132,600,likiwa na mamilionea 314 na mabilionea 25. Houston ni moja wapo ya miji inayokua kwa kasi zaidi ulimwenguni katika suala la ukuaji wa utajiri katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Pia ndilo jiji linaloongoza nchini Marekani katika sekta kadhaa muhimu ikijumuisha sekta ya anga, mahitaji muhimu (mafuta na gesi), kibayoteki, na uhandisi.
Beijing - mji mkuu wa mabilionea wa China
Mji mkuu wa China Beijing una mamilionea wakazi 131,500, wakiwemo mamilionea 363 na idadi kubwa ya mabilionea -44
Ni Jiji la New York pekee na eneo la San Francisco Bay ndio yana idadi ya juu kulingana na kipimo hiki. Beijing pia ina makao makuu ya makampuni makubwa zaidi ya China.
Shanghai - kituo cha fedha cha China
Shanghai ni jiji lenye watu wengi zaidi nchini China
Shanghai ni mji mkubwa zaidi wa China, unaoonekana sana kama mji mkuu wake wa kifedha na ni nyumbani kwa mamilionea 130,100, ikiwa na mamilionea 350 na mabilionea 42.
Soko la Hisa la Shanghai ni la tatu kwa ukubwa duniani kwa ukubwa wa soko (baada ya Dow Jones na NASDAQ).
Chanzo - BBC SWAHILI
Social Plugin