Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA BAADA YA KUMUUA MKEWE KISA KANYIMWA TENDO LA NDOA

Mshitakiwa Taitus Malambwa mwenye pingu akiwa anatoka nje ya Mahakama baada ya kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kumuua mke wake kwa mausudi baada ya kukasirishwa kufuatia kunyimwa tendo la ndoa.

Na Walter Mguluchuma - Malunde 1 blog Katavi


Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Taitus Malambwa (28) Mkazi wa Kijiji cha Ntibili Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mke wake kwa maksudi wakati wakiwa wamelala kitandani alipokasirika kufuatia kunyimwa na mkewe tendo la ndoa.


Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi Gway Sumaye mwenye mamlaka ya juu ya kusikiliza kesi za Mahakama kuu baada ya Mahakama kuridhika pasipo shaka yoyote ile kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo ukiwepo ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mama mzazi wa mshitakiwa pamoja na shangazi yake .


Mshitakiwa Taitus amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kifungu cha sheria Namba 196 na 197 cha kanunu ya adhabu .


Awali katika kesi hiyo mwendesha mashitaka mwanashria wa kutoka ofisi ya mashitaka Mkoa wa Katavi Hongera Malifimbo aliiambia Mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 3 Novemba 2019 huko katika Kijiji cha Ntibili Wilaya ya Mlele Mkoani hapa.



Siku hiyo ya tukio Titus Malambwa alikuwa amelala  chumbani na mke wake aitwaye Noelia Costa  na baada ya kufanya nae mke wake tendo la ndoa mara moja mshitakiwa hakuridhika alimwomba marehemu waendelee na tendo hilo la ndoa kwa mara nyingine tena jambo ambalo marehemu alikataa kuendelea kufanya tendo la ndoa kwa kudai kuwa amechoka.


Mwendesha mashitaka Hongera Malifimbo alieleza kuwa kitendo hicho cha marehemu kumnyima mume wake tendo la ndoa kilimkasirisha mshitakiwa na ndiyo aliposubiria mke wake ampate usingizi alitoka nje na kuchukua shoka na kumkata nalo kichwani ,tumboni na shingoni na kumsababishia majeraha makubwa yaliyomfanya atoke damu nyingi na kumsabisha kifo.


Baada ya kuwa ametekeleza mauaji hayo mshitakiwa alitoroka hadi alipokamatwa akiwa kwenye Kijiji cha Kakese kufuatia jitihada kubwa zilizofanywa na jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi.


Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi mfawidhi mwenye Mamlaka ya kusikiliza kesi za Mahakama kuu Gway Sumaye aliiambia Mahakama kuwa pasipo shaka yoyote ile kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo mshitakiwa ametiwa hatiani pasipo shaka yoyote ile .

Hivyo alitoa nafasi kwa wanasheria wa upande wa mashitaka na utetezi kama wanalo jambo lolote la kuileza Mahakama kabla ya hukumu kusomwa.


Mwanasheria wa Serikali Hongera Malifombo aliiomba Mahakama itoe adhabu kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza licha ya kuwa mshitakiwa huyo hakuwa na historia yoyote ya kufanya kosa jingine. .


Kwa upande wa mshitakiwa  mwanasheria wake Hamad Arfi alisema kuwa hana cha kuiomba Mahakama kwa kuwa kosa alilopatikana nalo mshitakiwa adhabu yake kwa mujibu wa sheria ni moja tu.


Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi Gway Sumaye mwenye mamlaka ya kusikiliza kesi za Mahakama kuu alisoma hukumu na kuiambia Mahakama kuwa mshitakiwa amepatikana na hatia kinyume na kifungu cha sheria namba 196 na 197 cha kanuni ya adhabu .


Kwa hiyo Taitus Malabwa Mahakama imemuhukumu kunyongwa hadi kufa na kama itahitaji kukata rufaa nafasi hiyo ya kukata rufaa ipo wazi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com