Picha haihusiani na habari hapa chini
***
MKULIMA wa Kijiji cha Mshikamano, Wilaya ya Nachingwea, Albert Mkuwele (49), amemuua kwa kumchinja kwa panga mpenzi wake, Rejina Sotti (46) kisha naye kujiua kwa kujikata koromeo.
Diwani wa Kata ya Mitumbati, Saimon Njende na Ofisa Mtendaji, Emmanuel Ndunguru, walisema wapenzi hao waliishi pamoja kama mke na mume kwa miaka 28 na kubahatika kupata watoto wanne na wajukuu wawili.
Alisema kabla ya mauaji hayo, wapenzi hao walionekana kutokuwa na maelewano mazuri kwa muda mrefu hali iliyomsukuma Mkuwele kuondoka na kwenda kuishi kijiji kingine.
“Wapenzi hawa hadi wanauana hawakuwahi kufunga ndoa na wameishi pamoja kwa miaka 28, wamebahatika kupata watoto wanne na wajukuu wawili,” alisema Diwani Njende.
Alisema siku ya tukio, mwanaume alirejea nyumbani na kuwakuta watoto alipowauliza alipo mama yao na kujibiwa kuwa yupo shambani akivuna mbaazi, alionekana akichukua panga huku akilinoa na kuelekea alipo mpenzi wake ambako alitekeleza mauaji hayo.
Taarifa zinasema kuwa alimkata shingo na kutenganisha kichwa na kiwiliwili, baadaye kugeuza panga alilolitumia kumjichinjia mzazi mwenzake, kujikata koromeo na kufariki papo hapo.
Chanzo - Nipashe
Social Plugin