Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam William Mkonda,a kionesha baaadhi ya vifaa walivyovikamata
***
Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam limemkamata Selemani Kalembo (57) maarufu kama Sele Bonge mkazi wa Vingunguti na wenzake 9 kwa tuhuma za kuvamia nyumba na kuiba vitu mbalimbali katika eneo la Kinyerezi, Kibaga mkoani Dar es Salaam ambapo walikamatwa wakiwa na gari aina ya Noah yenye namba T 218 BYS na vifaa mbalimbali vya kuvunjia nyumba, televisheni 4, kamba na mfuko wa kufichia TV baada ya kuiba.
.
Hata hivyo, Jeshi hilo limebainisha kuwa mahojiano ya kina yanaendelea ili kuwakamata wote wanaoshirikiana nao.
Social Plugin