Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camillus Wambura.
MKUU wa Jeshi la Polisi, IGP Camillus Wambura amewahamisha mikoa ya kazi baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa huku mmoja akimhamishia Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
Katika taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime, waliohamishwa ni Kamanda Henry Mwaibambe kutoka Geita kwenda Tanga, na Kamanda Safia Shomary aliyekuwa Tanga amehamishiwa Mkoa wa Geita.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Temeke, Richard Ngole amehamishiwa makao makuu na nafasi yake imechukuliwa na Kungu Malulu aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rufiji.
Social Plugin