Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KATAMBI AZINDUA ALBAMU YA TENDA WEMA YA SALOME NTALIMBO...BAHATI BUKUKU, NEEMA MWAIPOPO WATIKISA KANISA LA EAGT USHIRIKA SHINYANGA


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga akizindua Albamu ya Tenda Wema ya mwimbaji wa muziki wa nyimbo za Injili Salome Ntalimbo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Tenda Wema ya mwimbaji wa muziki wa nyimbo za Injili Salome Ntalimbo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga akimpongeza mwimbaji wa muziki wa nyimbo za Injili Salome Ntalimbo kwa Albamu ya Tenda Wema.

***

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga amezindua Albamu ya Tenda Wema ya mwimbaji wa muziki wa nyimbo za Injili Salome Ntalimbo.


Uzinduzi wa Albamu hiyo iitwayo Tenda Wema kutoka kwa Mwimbaji Salome Ntalimbo umefanyika Jumapili Septemba 4, 2022 katika Kanisa la EAGT Ushirika Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na Waimbaji mbalimbali akiwemo Mwimbaji wa nyimbo za Injili Bahati Bukuku ,Neema Mwaipopo pamoja na viongozi mbalimbali wa taasisi na serikali akiwemo Mfanyabiashara maarufu Gilitu Makula na Meneja msaidizi wa Benki ya Exim Tawi la Mwanza,Sarah Tito.


Awali akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi Mhe. Katambi, mwimbaji wa nyimbo za injili Salome Ntalimbo ameeleza kuwa ili afikie adhima yake anahitaji zaidi ya Shilingi milioni 45 kwa ajili ya kununua vyombo vya muziki ili aendelee kulitangaza neno la Mungu kwa njia ya kuimba ndani na nje ya nchi ya Tanzania.

Akizungumzia changamoto alizokutana nazo kwenye muziki huo, Salome Ntalimbo alisema ni gharama kubwa ya uandaaji wa nyimbo pamoja na kusambaza kazi hiyo.


“Naimba muziki kwa sababu nasikia kuitwa kwa ajili ya kazi hiyo, kusema kweli gharama za uandaaji wa kazi nzuri ni kubwa hata hivyo namshukuru Mungu kwa sababu nimeshakamilisha hatua ya kwanza,” alisisitiza Salome.


Hata hivyo alisema, imekuwa rahisi kwake kufikia ndoto ya mafanikio kwa sababu ya ushirikiano mkubwa kutoka kwa waimbaji waliomtangulia akiwemo Bahati Bukuku ,Neema Mwaipopo na waimbaji wengine.


Kufuatia risala hiyo, Mhe. Katambi ametoa pesa taslimu kiasi cha shilingi milioni 5 ,John Ntalimbo mme wa Salome akitoa shilingi Milioni 5 ,Gilitu Makula milioni 3,Bahati Bukuku Milioni 1 huku Meneja msaidizi wa Benki ya Exim Tawi la Mwanza Sarah Tito na wadau wengine wakichangia fedha zao ambapo kwa pamoja wamechangia pesa taslimu kiasi cha shilingi milioni 29 na ahadi Shilingi milioni 11 ,Jumla ahadi na deni wakifikisha Shilingi milioni 40.


Katambi alisema kuwa ameguswa na kazi ya Salome Ntalimbo na ndiyo sababu iliyomfanya kufika katika kanisa la EAGT Ushirika kwa ajili ya kumtia moyo mwimbaji huyo ambaye amedhamiria kuhubiri na kulitangaza neno la Mungu kwa njia ya kuimba.


Kwa upande wake John Ntalimbo akitoa neno la shukrani aliwashukuru wadau wote waliojitoa kuwezesha hafla hiyo na kueleza kuwa yeye akiwa mme wa Salome amemruhusu kumtumikia Mungu kwa moyo wake wote.

Askofu wa kanisa la EAGT Ushirika Askofu Raphael Machimu aliahidi kuendelea kumwombea mwimbaji Salome Ntalimbo ili azidi kuifanya kazi ya Bwana.
Askofu wa kanisa la EAGT Ushirika Askofu Raphael Machimu akiomba kabla ya Albamu ya Tenda Wema kuzinduliwa.
Askofu wa kanisa la EAGT Ushirika Askofu Raphael Machimu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Tenda Wema.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Tenda Wema ya mwimbaji wa muziki wa nyimbo za Injili Salome Ntalimbo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Tenda Wema ya mwimbaji wa muziki wa nyimbo za Injili Salome Ntalimbo.
Salome Ntalimbo na Bahati Bukuku wakiimba wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Tenda Wema
Salome Ntalimbo na Bahati Bukuku wakiimba wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Tenda Wema
Salome Ntalimbo na Bahati Bukuku wakiimba wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Tenda Wema
Neema Mwaipopo akiimba kanisani
Bahati Bukuku akitoa Fedha Milioni 1 kwa ajili ya kuunga mkono uzinduzi wa albamu ya Tenda Wema
John Ntalimbo akiwa na mke wake Salome Ntalimbo wakati  wa uzinduzi wa albamu ya Tenda Wema
John Ntalimbo akieleza furaha yake baada ya  mke wake kuzindua Albamu ya Tenda Wema
Meneja  msaidizi wa Benki ya EXIM tawi la Mwanza Sara Tito akiwa na wahandisi wa TARURA

Bahati Bukuku ,Salome Ntalimbo na Neema  Mwaipopo wakiwa wamekaa pamoja.
Bahati Bukuku ,Salome Ntalimbo na Neema  Mwaipopo wakiwa wamekaa pamoja.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com