Serikali ya Tanzania imetangaza kuanza kuchukua hatua kali kwa watu watakaobainika kusambaza maudhui yanayohamasisha mapenzi ya jinsi moja huku ikiwatahadharisha viongozi wa makundi ya WhatsApp Ma ‘admin’ ambao hawatafuata au kuchukua hatua kwa wanaosambaza maudhui ya mapenzi ya jinsi moja yakiambatanishwa na video au picha.
Akizungumza leo Jumapili Septemba 11, 2022 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye jijini Dar es Salaam amesema hatua hiyo imekuja kufuatia kukithiri kwa vipande vya video zinazosambaa mitandaoni zikionyesha vitendo vya aina hiyo.
"Sasa nitoe tahadhari tutakapoanza kuwazoa, hatutegemei taharuki maana hadi mimi kujitokeza kuzungumzia hili suala ni wazi kwamba tumeamua kulifanyia kazi. Kuweni makini huko kwenye mitandao na makundi ya WhatsApp hasa ma admin hatuna utani katika hili, Picha na video zinasambaa kupitia mitandao ya kijamii hasa makundi ya WhatsApp", amesema Waziri Nape.
Social Plugin