Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JONATHAN MADETE ACHAGULIWA KWA KISHINDO NAFASI YA MWENYEKITI WA UVCCM SHINYANGA MJINI

Kulia ni Jonathan Madete akisalimiana na katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Ally  Majeshi baada ya uchaguzi
Jonathan Madete

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jonathan Madete  amechaguliwa kwa kishindo kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini akipata kura 127 na kufuatiwa na Hashimu Issa aliyepata kura 49 na Chiku Gidioni kura 67.

Wajumbe wa mkutano mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (uCCM)  wilaya ya Shinyanga mjini leo Ijumaa Septemba 23,2022 wamefanya uchaguzi   wa viongozi mbalimbali akiwemo kumchagua mwenyekiti wa UVCCM wilaya na wajumbe mbalimbali.

Jonathan Madete anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Dotto Joshua



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com