Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Fatuma Omary Latu na dereva wake amefariki dunia leo katika ajali iliyotokea katika eneo la Shamwengo, Inyala mkoani Mbeya.
Ajali hiyo imetokea leo Septemba 14, 2022, ambapo Mkurugenzi huyo alikuwa anatoka kwenye mkutano mkuu wa 36 wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa (ALAT), uliofanyika jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa chanzo cha ajali hiyo, ni uzembe wa dereva wa gari la mkurugenzi aliyekaidi amri ya jeshi la polisi kusimama ili kupisha msafara wa malori.
Ajali hiyo imehusisha pia magari mengine mawili, likiwemo lori la kubebea mafuta, mali ya kampuni ya Lake Oil na lori lingine la mizigo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, aliyefariki dunia
Social Plugin