Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI ...MHANDISI KHATIB APELEKWA TCRA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

  1. Amemteua Bw. Sosthenes Laurent Kewe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Tanzania (TIB). Bw. Kewe ni Mshauri Binafsi wa Uendelezaji wa Sekta Binafsi za Fedha, Dar es Salaam.

2.Amemteua Mhandisi Othman Sharif Khatib kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Bw Khatib anachukua nafasi ya Dkt. Jones Kilembe ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Bw. Khatib ni Mhandisi Mstaafu (TCRA).

3.Amemteua Dkt. David Nkanda Manyanza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI). Dkt. Manyanza ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Development Solution Consultancy (T) Limited.

4.Amemteua Bi. Hawa Abdulrahman Ghasia kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko Kariakoo. Bi Ghasia ni Mbunge mstaafu.

5.Amemteua Bw. Sylvester Jospeh Kainda kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani. Bw. Kainda ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Morogoro.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com