Binti mmoja mwenye umri wa 21 anayejulikana kwa jina la Rehema Musa mkazi wa Mtaa wa Ilindi Kata ya Zongomera wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ambaye ni mlemavu wa viungo vya mwili anapitia changamoto nyingi baada ya kutelekezwa na Baba yake Mzazi zaidi ya miaka 20.
Akizungumza na Huheso Digital Tv Amina Imamu Kibila
ambaye ni Mama mzazi wa Binti huyo ameelezea kwa uchungu kuhusiana na
changamoto ambazo anazipitia binti yake
ambapo baadhi ya ndugu zake wamemtenga
mama huyo wakiamini kuwa ameleta mkosi kwenye ukoo wao.
Mama mzazi wa binti huyo ameeleza kuwa anapata changamoto kubwa ya
kumhudumia Binti yake maana yeye
mwenyewe hana kipato chochote cha kukidhi mahitaji yake na anaishi katika mazingira magumu ikiwemo kukosa mahali pa kuishi.
Baadhi ya majirani wa eneo hilo Monica Richard na Sande Buluba wamezungumzia Maisha halisi ya
Binti huyo kuwa anapata shida sana maana
hawezi kufanya kitu chochote mfano kutembea,
kuzungumza, kula, kufua, n.k
Kwa upande wake mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Ilindi Ndg Dogo Mheziwa ametoa wito kwa
jamii kuacha tabia ya kuwatenga watu wenye ulemavu na kuondokana na imani
potofu kuwa ulemavu siyo mkosi bali ni mpango wa Mungu jamii inatakiwa kuwajali na kuwapa nafasi
Ukiguswa na unahitaji kumsaidia tafadhali wasiliana na Mama Rehema kwa Namba 0753-367-865 na 0688-598-292.
Ukiitaji kumsaidia Rehema tafadhali namba zake hizo hapo juu pia unaweza kutuma Msaada wako kupitia akaunti
0150059582900 - Huheso CRDB bank
Pata muda uangalie masaibu anayopitia Rehema na Mama yake katika kumtunza baada ya kutelekezwa na Baba yake miaka 21 iliyopita.
Social Plugin