Na John Walter-Manyara
Watu saba wamefariki dunia na wengine Kumi na nne wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani baada ya gari dogo la abiria kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Cheka nao kata ya Kiperesa wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Akizungumza na Waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara George Katabazi, amesema ajali hiyo imetokea Septemba 19 majira ya saa 12:00 asubuhi ambapo watu sita walifariki papo hapo na mmoja alifariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
Kamanda amesema gari hilo lenye namba za usajili T 266 APM aina ya Mitsubish Mini Bus linafanya safari zake Kutoka Matui Kiteto kwenda Kondoa mkoani Dodoma.
"Gari hilo mini bus lililokuwa linatokea Matui lilipata ajali eneo la Chekanao kata ya Kiperesa wakati likielekea Wilayani Kondoa mkoani Dodoma" amesema Katabazi.
Katabazi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva uliosababisha gari hilo kuhama njia na kupinduka ambapo baada ya tukio Dereva huyo aliejulikana kwa jina moja la Nurdin alikimbia.
Social Plugin