TAASISI YA JAKAYA MRISHO KIKWETE NA PLAN INTERNATIONAL WAANDAA MAFUNZO YA KUJENGA UWEZO KWA WATOTO WA KIKE KUJIAMINI

                       TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

22nd September 2022

 

“TAASISI YA JAKAYA MRISHO KIKWETE NA PLAN INTERNATIONAL WAANDAA MAFUNZO YA KUJENGA UWEZO KWA WATOTO WA KIKE KUJIAMNINI”

 

 

KAULI MBIU: ‘’Wakati wetu ni sasa—haki zetu, mustakabali wetu”

 

DAR ES SALAAM SEPTEMBER 21, 2022: Taasisi za Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) na Plan International Tanzania zimeandaa mafunzo ya kuongeza uwezo wa kujiamini kwa  watoto wa kike 40 juu ya kutambua afya ya akili, kukuza ustawi wao hususan katika masuala ya lishe na ukakamavu, haki za mtoto wa kike pamoja na ufahamu wa sheria za nchi juu ya maswala hayo.


Mafunzo hayo, ni sehemu ya shughuli za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike duniani, yatafanyika mnamo Septemba 24, 2022 katika hoteli ya Regency jijini Dar es salaam. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni imelenga ile ile ya kimataifa ya: “Wakati wetu ni sasa—haki zetu, mustakabali wetu”

 

“Mafunzo hayo yataenda kwa jina la “Wasichana Washika Hatamu” na ni jukwaa lakuwapa mafunzo Watoto wa kike ya kuongeza uwezo wa kujiamini ,kutambua afya ya akili, kukuza ustawi wao hususan katika masuala ya lishe na ukakamavu, haki za mtoto wa kike pamoja na ufahamu wa sheria za nchi katika nafasi za kufanya maamuzi”, anasema Mtendaji Mkuu wa JMKF, Bi. Vanessa Anyoti.

 

Bi Anyoti anaeleza kwamba Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike imekuwa jukwaa muhimu katika kutambua haki za msichana pamoja na changamoto kubwa anazopambana nazo duniani, na kwamba sasa kuna wito wa kuchukuliwa kwa hatua za maksudi za kuleta mageuzi  kijamii na kisiasa ili kuondoa vizuizi mbalimbali vya ubaguzi na chuki vinavyoendelea kurudisha nyuma maendeleo ya wasichana.

 

“Tanzania inaungana na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa katika kukuza ufahamu wa jamii juu ya masuala yanayowakabili wasichana na kuwapatia fursa ya kupaza sauti zao.

 

“Duniani, wasichana wanaendelea kukabiliana na changamoto za uongozi, elimu, masuala ya afya ya akili na ukatili wa kijinsia, wakati wao ndio mawakala wakuu wa mabadiliko katika jamii zao”, anaongezea Bi. Anyoti.

 

Kwa Habari zaidi wasiliana na Beatrice Mnzava via 0764065164 na  beatrice.mnzava@jmkfoundation.org

 


Muhidin Issa Michuzi

AFISA MAWASILIANO

JAKAYA MRISHO KIKWETE FOUNDATION


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post