Pete
Baada ya kusambaa kwa video mitandaoni zikionesha watalii wa jinsia ya kiume kuvishana pete hadharani, Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, imelaani vikali kitendo hicho kwani ni ukiukwaji wa sheria na kwamba uchunguzi unaendelea na hatua stahiki zitachukuliwa.
Katika andiko la Wizara hiyo limebainisha kuwa tukio hilo limetokea katika fukwe ya hoteli ya The Loop iliyopo Jambian, wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini Unguja, na wizara kwa shirikiana na kamisheni ya utalii imesema kwa sasa vyombo vya husika vya serikali vinaendelea na uchunguzi na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wote walioandaa, kusimamia na waliohusika na tukio hilo.
Sintofahamu kwa jamii ya Kizanzibar hata taasisi nyingine za dini, ambapo pia zimekemea kitendo hicho ikiwa ni pamoja na ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar imelazimika kutoa andiko kukemea tukio hilo.
Chanzo - EATV
Social Plugin