Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amesema hapendi kuona mabango yanayotangaza kuongeza nguvu za kiume au kusafisha nyota sambamba na matangazo mengine yanayofanana na hayo katika maeneo ya mkoa huo badala yake anataka kuona mabango yanayohusu elimu ili kuongeza taaluma kwa wanafunzi.
Mtaka amebainisha hayo wakati akizungumza na wakuu wa shule pamoja na maafisa elimu wa mkoa huo katika hafla ya uzinduzi wa kifurushi maalumu kilichotolewa na benki ya NMB kwa ajili ya kuwasaidia walimu kuepukana na mikopo umiza.
“Unaenda kwenye mitaa unakuta bango tunasifisha nyota,hivi tuko siliasi! Hapana tusiende huko mimi nataka nikipita barabarani nione bango kubwa Pre-Form One, haya ndio ninayoyataka kuona”,amesema Mtaka
Social Plugin