Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BINTI ALIYEPOOZA MWILI MZIMA ABAKWA




Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Juma Ligamba (45), mkazi wa Kijiji cha Kibubwa, Kata ya Butuguri wilayani Butiama mkoani Mara anadaiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni mlemavu aliyepooza mwili mzima tangu kuzaliwa kwake.

Akisimulia kwa masikitiko tukio hilo la kubakwa kwa binti yake mama mzazi wa mtoto huyo anasema binti yake ana ulemavu huo unaomfanya muda wote kulala tu kwani alipooza mwili akiwa na wiki tatu tangu alipozaliwa kwake.

Nae Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Butiama, Devotha Paschal, amesema kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na kukithiri kwa vitendo vya ukatili wilayani humo huku mwanaasheria kutoka asasi isiyo ya kiserikali ya ATFGM Masanga Irene Assey, akikemea vikali juu ya vitendo hivyo vya ubakaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibubwa anasema alipata taarifa ya tukio hilo la ubakaji na kushirikiana na familia katika kumkamata mhalifu ambaye yupo chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi kwa sasa na uchunguzi unaendelea.

Naye, Adventina Victor ambaye ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya amekiri kumpokea mwathirika wa tukio hilo aliyefikishwa hospitalini hapo baada ya tukio hilo la kikatili na kusema kuwa anaendelea na matibabu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com