ANNE MAKINDA : SENSA IMEKUWA YA KIPEKEE, WANANCHI WALIKUWA NA UZALENDO KWA NCHI YAO

 

Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi (2022)Anne Makinda akizungumza kwenye kikao na wajumbe wa Kamati ya Sensa Mkoa wa Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KAMISAA wa Sensa ya watu na Makazi 2022 Anne Makinda, amesema zoezi la Sensa ya watu na makazi ambalo limefanyika Agosti 23 mwaka huu lilikuwa na uzalendo, na kusababisha kufanyika kwa ukamilifu na kufikia malengo yaliyokusudiwa.


Makinda amebainisha hayo leo Septemba 20, 2022 mkoani Shinyanga, kwenye kikao cha Kamati ya Tathmini ya Sensa mkoani humo.

Amesema Sensa ya mwaka huu 2022 ilikuwa ya kipekee, ambapo wananchi walikuwa na uzalendo na nchi yao, na kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa na kusababisha zoezi hilo kufanikiwa.

“Sensa ya mwaka huu 2022 ilikuwa na uzalendo, watu wengi wamejitokeza kuhesabiwa, na takwimu za kujua watanzania kwa sasa tupo wangapi mara baada ya zoezi hili kumalizika zitatolewa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan,”amesema Makinda.

“Nawapongeza pia viongozi wa dini, wanasiasa, wasanii, Waandishi wa habari na viongozi mbalimbali wakiwamo Wakuu wa Mikoa na Wilaya, kwa kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa Sensa kwa manufaa ya maendeleo yao,”ameongeza.

Aidha, amesema katika mapungufu yaliyojitokeza kwenye Sensa ya mwaka huu 2022 likiwamo la Migogoro ya mipaka ambalo limeonekana kuwa tatizo kwenye maeneo mengi lifanyiwe kazi ili Sensa ya mwaka 2032 lisiwepo.

Kwa upande wake Mratibu wa Sensa ya watu na Makazi mkoani Shinyanga Eliud Kamendu, amesema mkoani humo wamefanikiwa kwenye zoezi la Sensa kwa zaidi ya asilimia 100.

Amesema walikuwa na Makadirio ya kuhesabu Kaya 387,948, lakini wamehesabu Kaya 424,312, kwa upande wa Makazi Makadirio ni kuhesabu Majengo 325,235, na wakahesabu Majengo 409,342.

Ametaja baadhi ya matatizo ambayo walikumbana nayo kwenye kuhesabu Sensa, kuwa ni Migogoro ya Mipaka na kusababisha wananchi wa maeneo hayo yenye migogoro kugoma kuhesabiwa, lakini walitatua tatizo wakawahesabu, Vishikwambi kuwa na matatizo ya kuhifadhi umeme, Mitandao kutopatikana baadhi ya maeneo na kuchelewa kwa vitendea kazi. Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi (2022)Anne Makinda akizungumza kwenye kikao na wajumbe wa Kamati ya Sensa Mkoa wa Shinyanga.


Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi (2022)Anne Makinda akizungumza kwenye kikao na wajumbe wa Kamati ya Sensa Mkoa wa Shinyanga.

Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi (2022)Anne Makinda akizungumza kwenye kikao na wajumbe wa Kamati ya Sensa Mkoa wa Shinyanga.

Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi (2022) Anne Makinda akizungumza kwenye kikao na wajumbe wa Kamati ya Sensa Mkoa wa Shinyanga.

Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi (2022)Anne Makinda akizungumza kwenye kikao na wajumbe wa Kamati ya Sensa Mkoa wa Shinyanga.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof Siza Tumbo, akizungumza kwenye kikao hicho.

Mratibu wa Sensa ya watu na Makazi mkoani Shinyanga Eliud Kamendu, akitoa taarifa ya Sensa mkoani humo.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi (2022)Anne Makinda, akipiga picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Sensa Mkoa wa Shinyanga.

Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi (2022) Anne Makinda, akipiga picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Sensa Mkoa wa Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post