MAKINDA : HAKUNA ATHARI YA WAKIMBIZI KWENYE ZOEZI LA SENSA


Kamisaa wa sensa ya watu na makazi nchini Anne Makinda (wa pili kulia) akizungumza na waratibu wa zoezi la sensa ya watu na makazi wa halmashauri ya wilaya Kigoma alipofanya ziara kutembelea na kukagua maendeleo ya zoezi hilo katika kijiji cha Kalalangabo Halmashauri ya wilaya Kigoma.
**

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

KAMISAA wa sensa ya watu na makazi Anne Makinda amesema kuwa licha ya kuwepo kwa idadi kubwa ya wakimbizi kwenye kambi mbalimbali mkoani humo hakujaathiri zoezi la ukusanyaji wa takwimu za idadi ya watu katika maeneo mbalimbali ya mkoa Kigoma.

Akizungumza mkoani Kigoma kwenye siku ya pili ya ziara yake mkoani Kigoma kutembelea na kukagua maendeleo ya zoezi la sensa ya watu na makazi Makinda amesema kuwa zoezi limefanyika vizuri na lengo lililowekwa limefikiwa.

Alisema  wakimbizi kwenye makambi wanayohifadhiwa wanazo taratibu zao za kuchukua takwimu za idadi ya watu na kwamba zoezi hili la sense ya kitaifa halijaathiriwa na uwepo wao na kwamba kila mmoja atahesabiwa na kufikiwa kulingana na taratibu zlizowekwa.

Makinda alisema zipo taarifa za kuwepo kwa watu katika maeneo yasiyo rasmi wakiwemo wafugaji wanaohama hama serikali imeweka mkakati kuhakikisha wanafikiwa na matangazo yamewekwa kila mahali kuwataka watoe taarifa walipo na watafikiwa na makarani wa kukusanya takwimu.

Kamisaa huyo wa Sensa Taifa amewashukuru viongozi wa mitaa, vijiji na vitongoji ambao wametoa ushirikiano mkubwa kwa kuwaonyesha maeneo na kutembea na baadhi ya makarani na kwamba kazi waliyofanya ni ya uzalendi mkubwa na mchango wao unatambuliwa.

Kwa upande wake Meneja wa ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mkoa Kigoma, Moses Kahero alisema kuwa alisema kuwa hakuna changamoto kubwa zilizojitokeza wakati wa zoezi hilo na kwamba watu wote walio kwenye maeneo rasmi wamefikiwa na kuhesabiwa.

Kahero alisema kuwa zipo taarifa za uwepo wa watu kwenye maeneo yasiyo rasmi hasa wafugaji wanaohama tayari utaratibu umewekwa na wanafuatiliwa kuhakikisha watu wote wanafikiwa na kuhesabiwa.

Meneja huyo wa NBS mkoa Kigoma alisema kuwa kumekuwa na mwamko kwa wananchi ambao hawajafikiwa kujitokeza na kupiga simu ambapo wametoa maelekezo maeneo yaliyopo na kuhesabiwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post