Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo (kulia) akiendesha mijadala katika semina maalum kwa waandishi wa habari, iliyopewa jina la “CRDB Bank Media Day” iliyolenga kuwajengea uwezo na ujuzi waandishi wa habari za biashara na uchumi ili kuweza kutekeleza majukumu yao ya kuihabarisha jamii.
Pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communication Ltd, Bakari Machumu, Mkuu wa Idara ya Huduma ya Radio TBC, Asha Mbaruku, na Mhadhiri Chuo Kikuu Dar es salaam, Dkt. Darius Mukiza.
Katika jitihada za kuendeleza sekta ya habari nchini, Benki ya CRDB imeendesha semina maalum kwa waandishi wa habari za biashara na uchumi iliyofanyika katika Makao Makuu ya benki hiyo yaliyopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa amesema semina hiyo iliyopewa jina la “CRDB Bank Media Day” imelenga kuwajengea uwezo na ujuzi waandishi wa habari ili kuweza kutekeleza majukumu yao ya kuihabarisha jamii kwa ufanisi na waledi mkubwa.
Semina hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam leo Jumanne Septemba 20,2022 na kuhudhuriwa na zaidi ya waandishi 200 kutoka vyomb o mbalimbali nchini.
“Tukiwa wadau wakubwa wa sekta ya habari tuna jukumu la kuhakikisha waandishi wa habari wanafanya kazi yao vizuri kwa kuwaongezea maarifa yatakayowasidia kuandaa na kuhariri habari za biashara na uchumi kwa weledi mkubwa,” alisema Mwambapa.
Mwambapa alisema Benki hiyo imeona kuna pengo linaloongezeka la ubora wa habari za biashara na fedha kwenye vyombo vya habari msukumo uliopelekea kuandaa semina hiyo. Aliongezea kuwa mpango ni kuendelea kuandaa semina hiyo mara kwa mara ili kuinua kiwango cha taarifa za fedha.
Mkurugenzi huyo alisema mafanikio ya Benki ya CRDB yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na taarifa za vyombo vya habari kwa umma ambazo zilikuwa na matokeo chanya kwa jamii.
"Vyombo vya habari sio tu vimesaidia kutangaza huduma na malengo ya Benki ya CRDB lakini pia utendaji wa uchumi wa taifa katika hatua mbalimbali," alisema.
Alisema licha ya sera nzuri za uchumi za nchi kama vyombo vya habari vitapuuzwa malengo ya kuwawezesha watu kufahamu kinachoendelea katika mazingira yao na fursa zilizopo hayataweza kufikiwa.
Kutokana na umuhimu wa vyombo vya habari kuinua sekta mbalimbali za uchumi benki hiyo sasa imepania kuendelea kufadhili waandishi wa habari hususan katika tafiti zinazohusu masuala ya uchumi, fedha na taarifa za biashara ili kuwafikia wananchi wengi.
Akichangia mjadala wa “Jukumu la Vyombo la Habari katika Kukuza Uchumi” Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications, Bakari Machumu, aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa semina hiyo kwa waandishi wa habari.
Machumu alisema waandishi wa habari wanapaswa pia kujenga uelewa wa kutosha wa sekta mbalimbali jambo litakalowasidia katika kujenga hoja katika taarifa zao.
"Kujenga uelewa juu ya sekta husika kutamwezesha mtu sio tu kuandika taarifa bora bali pia kujenga uwezo wa kuhoji kutakakowezesha kupata taarifa zaidi," Bw Machumu, ambaye pia ni mtaalamu wa habari za biashara, alisema wakati wa kongamano hilo.
Menejea Mwanadamizi wa PwC, Samwel Carol akiwasilisha mada kuhusu namna ya kuripoti taarifa za fedha alisema mtu anapaswa kusoma na kusoma na kusoma tena taarifa hiyo na akishindwa kuelewa aliwaomba kuuliza kwa wataalamu ili kuweza kuripoti taarifa kwa usahihi.
Kwa upande wa fursa za habari katika mitandao ya kijamii, Stephen Mokiwa mwanzilishi wa Teknkona, alisema vyombo vya habari vinapaswa kutengeneza bidhaa za kidijtali ili kuendana na mbadiliko ya walaji wa habari.
Alipongeza baadhi ya vyombo kuanza kuchangamkia katika upande huo.
Mada mbalimbali zimewasilishwa katika semina hiyo ikiwamo Uwasilishaji wa Habari za Taarifa za Fedha iliyowasilishwa na Meneja Mwandamizi PwC Samwel Karoli, Fursa za Mitandao ya Kijamii katika Sekta yaHabari iliyowasilishwa na Stephen Mokiwa mwanzilishi wa kampuni ya Teknkona, huku mwanahabari maarufu wa mitandao Millard Ayo akichangia kupitia mtandao.
Mada zingine zilikuwa ni kanuni za utangazaji katika kuandaa vipindi na habari za uchumi na biashara iliyowasilishwa na Rolf Kibaja Mtaalam wa Maudhui TCRA, pamoja na mada ya Maadili ya Uandishi wa Habari iliyowsilishwa na Dkt. Darius Mukiza Mhadhiri Chuo Kikuu Dar es salaam.
Mtaalam wa Maudhui kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Rolf Kibaja akizungumza katika semina maalum kwa waandishi wa habari, iliyopewa jina la “CRDB Bank Media Day” iliyolenga kuwajengea uwezo na ujuzi waandishi wa habari za biashara na uchumi ili kuweza kutekeleza majukumu yao ya kuihabarisha jami.
Mhadhiri Chuo Kikuu Dar es salaam, Dkt. Darius Mukiza akizungumza katika semina maalum kwa waandishi wa habari, iliyopewa jina la “CRDB Bank Media Day” iliyolenga kuwajengea uwezo na ujuzi waandishi wa habari za biashara na uchumi ili kuweza kutekeleza majukumu yao ya kuihabarisha jami.
Meneja Mwandanimizi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo akizungumza wakati akiendesha mijadala katika semina maalum kwa waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile akichangia mjadala wa “Jukumu la Vyombo la Habari katika Kukuza Uchumi” katika semina maalum kwa waandishi wa habari, iliyopewa jina la “CRDB Bank Media Day” iliyolenga kuwajengea uwezo na ujuzi waandishi wa habari za biashara na uchumi ili kuweza kutekeleza majukumu yao ya kuihabarisha jami.
Social Plugin