Kishikwambi
***
Jeshi la Polisi mkoa wa Geita linaendelea kukitafuta kishikwambi kilichoibiwa kwenye nyumba ya kulala wageni wilayani Chato mkoani Geita huku kimoja kilichoibiwa wilayani Mbogwe kikikamatiwa mkoani Singida.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Geita Ally Kitumbu, amethibitisha kuibiwa kwa vishikwambi huku wakiendelea na jitihada za kutafuta kilichoibiwa wilayani Chato.
"Afisa wa Sensa kutoka bila kufunga mlango ndipo watu wasiofahamika wakaingia mule na kuweza kuiba kile kishikwambi, hadi sasa juhudi za kutafuta zinaendelea lakini tunaamini kwamba baada ya muda mfupi kitakuwa kimepatikana," amesema Kamnada Kitumbu.
Aidha Kamanda Kitumbu ameongeza kuwa, "Kule wilayani Mbogwe kimepatikana baada ya Jeshi la Polisi mkoa wa Geita kwa kushirikiana na wenzetu na kukipata kule mkoani Singida kikiwa kimetelekezwa kwenye nyumba ya kulala wageni".
CHANZO - EATV
Social Plugin