Kisu
Askari mgambo Fred William (47), mkazi wa Kijiji cha Mkengwa, Rorya mkoani Mara, amefariki dunia baada ya kuchomwa na kisu shingoni akiwa katika kituo cha polisi Mkengwa, wakati akimzuia aliyemchoma kisu kutomfanyia fujo mke wake aliyekimbilia kituoni hapo kuomba msaada.
Tukio hilo limetokea Agosti 30, 2022, ambapo marehemu alikuwa akimzuia mtuhumiwa kutomfanyia fujo mke wake aliyekimbilia kituoni hapo kuomba msaada kutokana na kwamba walikuwa na ugomvi na alikuwa akitaka kumuua.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema marehemu alichukua jukumu hulo kutokana na kwamba Askari Polisi wa kituo hicho walishindwa kumdhibiti mtuhumiwa kwani hawakuwa na silaha ya aina yoyote.
Chanzo - EATV
Social Plugin