Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amehitimisha ziara yake mkoani Mwanza kwa kuzunguzumza na wanachama wa Chama hicho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ambaye amekuwa na Kinana kwenye mikoa yote aliyofanya ziara.
Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Dialo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula, wabunge, wajumbe wa NEC,,Mku wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima pamoja na wanachama wengine wa Chama hicho.
Akizungumza na Wana CCM hao Kinana amewahimiza kuendelea kudumisha umoja na mshikamano huku akikumbusha kuwa kwa sasa Chama kipo kwenye mchakato wa kuchagua viongozi hivyo ni vema wakachagua viongozi wenye sifa za uongozi badala ya kuchagua kwa kuangalia urafiki, ukabila au ukanda.
Katika ziara hiyo Kinana ametembelea mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita na Mwanza ambapo pamoja na mambo mengine amekutana amekagua miradi ya maendeleo ukiwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akizungumza na Viongozi wa Chama, Serikali pamoja na Wanachama wa CCM wakati wa kuhitimisha ziara yake mkoani Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
Picha mbalimbali zikimuonesha Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi wa Chama, Serikali pamoja na Wanachama wa CCM wakati wa kuhitimisha ziara yake mkoani Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
Social Plugin