Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BIBI WA MIAKA 86 ATEKETEZWA KWA MOTO CHUMBANI MAJAMBAZI WAKIIBA

Hali ya majonzi imeghubika familia moja katika kijiji cha Koinange katika wadi ya Gathabai, Kaunti ya Nyandarua nchini Kenya baada ya mwanamke wa miaka 86 kuteketezwa chumbani katika nyumba yake.

Inashukiwa kuwa moto huo ulianzishwa na majambazi ambao waliiba runinga, betri na meko ya gesi.

 Mjukuu wake kwa jina Jacob Wangondu aligundua mwili wa Grace Wanja nyumbani kwake Jumatatu.

 Mwili wake ulipelekwa katika makafani ya Hospitali ya Engineer huku polisi wakianzisha uchunguzi katika kifo hicho.

CHANZO-TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com