Amina Hassan, aliyechomwa visu hadi kufariki
**
Amina Hassan (34), mkazi wa mtaa wa Lukilini, Kata ya Kalangalala, amefariki dunia akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Geita baada ya kuchomwa visu zaidi ya mara 10 na mme wake usiku wa Agosti 30, 2022, na ameacha watoto wawili wa kike.
Baadhi ya majirani wamesema wanandoa hao walikuwa na mgogoro juu ya kukutana kimwili ambapo walishauriwa na daktari wasikutane kwa muda kutokana na changamoto za kiafya zinazowakabili, hivyo mwanaume alikataa ushauri wa daktari na amekuwa akitumia nguvu kumuingilia mkewe.
Majirani wanasema wawili hao walikuwa wametengana vyumba vya kulala kutokana na mwanaume alikataa ushauri wa kutumia dawa walizoshauriwa na madaktari.
Akizungumza kwa machungu mtoto wa marehemu ameelezea mara ya mwisho alivyokuwa anaangalia TV na mama yake mpaka kupitiwa na usingizi na ghafla akashtuka na kumkuta baba yake anampiga na kumchoma na visu mama yake sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo tumboni, chini ya kifua mbavuni na mgongoni mpaka kisu kilipomkatikia mwilini ndiyo akafungua mlango wa nyumba na kukimbia kusikojulikana.
CHANZO - EATV
Social Plugin