MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amefanya mabadiliko madogo ya kuwahamisha baadhi ya Makamanda wa Polisi, ambapo amemhamisha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya kwenda Makao makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Benjamini Kuzaga.
Taarifa hiyo imetolewa jijini Dodoma leo Septemba 13, 2022 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Makao Makuu ya Polisi, David A. Misime - SACP kwenye taarifa ya vyombo vya habari.
Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa , IGP Wambura amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) George Katabazi kutoka Makao makuu ya Upelelezi Dodoma kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Benjamini Kuzaga aliyehamishiwa kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya.
imeeleza kuwa Mabadiliko hayo ambayo yalianza tarehe 08.09.2022 ni katika kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Polisi.
Social Plugin