Bibi mwenye umri wa miaka 87 anayefahamika kwa jina la Elina Nzilano mkazi wa mtaa wa Idofi halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe ameuawa na mwanae mwenye ulemavu wa macho (Kipofu) anayefahamika kwa jina Elisha Mwena (42) huku sababu ikitajwa kuwa ni kikongwe huyo kumnyima chakula.
Kwa mujibu wa ripoti ya awali ya jeshi la polisi inasema mlemavu huyo wa macho ambaye ni mtoto wa bibi huyo alikasirishwa na kitendo chake cha kumyima mwanae chakula na sabafubu kubwa ya kutompa chakula ni mjukuu wake kuiba kuku wake na kumla.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi Hamis Issa amesema Mlemavu huyo wa macho alimshambulia mama yake baada ya mtoto wake kutopewa chakula kwasababu ya kuiba kuku wa bibi huyo na kisha kumla jambo ambalo likamkasirisha na kisha kuanza kumpa kichapo kwa fimbo bibi huyo na kumsababishia kifo.
Katika tukio jingine Jeshi la Polisi mkoani Njombe linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kuvamia katika mradi wa ujenzi wa chuo cha VETA cha mkoa wa Njombe unaotekelezwa katika kijiji cha Shaurimoyo wilayani Ludewa na kusababisha mauaji ya mlinzi anayefahamika kwa jina la Romanus Galus na kisha kuiba vifaa vya ujenzi
Mara baada ya mauaji hayo,Ndipo kituo hiki kikafanya mahojiano na msimamizi wa mradi Adam Rogers na Mbunge wa Ludewa Joseph Kamonga na mlinzi mwenza wa marehemu .
Chanzo - EATV
Social Plugin