MABASI YAENDAYO MIKOANI YARUHUSIWA KUINGIA KWENYE STENDI BINAFSI DAR


Na  James lyatuu, Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametangaza kuondoa katazo lililokuwa likizuia Mabasi yaendayo mikoani na nje ya Nchi kutoruhusiwa kupakia abiria au kushusha katika Vituo binafsi na badala yake ameruhusu utaratibu huo kuendelea kwa sharti la kila basi kuingia ndani ya Kituo kikuu cha Mabasi cha Magufuli.

RC Makalla ametoa maamuzi hayo wakati wa kikao cha pamoja baina ya LATRA, Wamiliki wa Stendi binafsi na Halmashauri ya Ubungo na kubaini pasipokuwa na shaka kuwa waliotengeneza Vituo binafsi walifuata taratibu na kupatiwa vibali na LATRA baada ya kukidhi vigezo.

Miongoni mwa vigezo vilivyotolewa na LATRA ili kuruhusiwa kuanzisha Stendi binafsi ni pamoja na uwepo wa Vyoo, Sehemu ya mapumzimo kwa abiria, viburudisho na sehemu ya maegesho.

Kutokana na  Makalla ameridhia Vituo binafsi 5 vilivyohakikiwa kuendelea kutoa huduma na kufungua milango kwa wamiliki wengine wanaohitaji kuwa na Vituo binafsi kushirikiana na LATRA ili wapatiwe vigezo vinavyohitajika ambapo wamepewa Mamlaka ya kufuta au kutoa leseni.

Aidha Makalla ameagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kukaa kikao mara moja na wamiliki wa Stendi binafsi ili kuona njia bora ya ukusanyaji wa mapato.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post