Na Richard Mrusha - Geita
Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Madini Msafiri Mbibo ametembelea Banda la Gf Truck Group lililopo kwenye maonyesho ya tano ya madini yanayoendelea mkoani humo huku akisifu namna kampuni hiyo ilivyojipanga katika kusaidia wachimbaji wadogo wadogo na wa kati.
Akiwa katika banda hilo Naibu katibu mkuu huyo Mbibo alipata fursa ya kupata maelezo kutoka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, ndugu Smart Deus pamoja na Meneja Mauzo Paul Msuku juu ya ushiriki wao kwenye maonyesho hayo na namna walivyojipanga katika kufikisha huduma zao kwa jamii.
Akitoa maelezo hayo leo Septemba 28 mwaka huu Meneja mawasiliano huyo, Smart Deus amesema kuwa wao kama kampuni,moja ya huduma ambazo wanazitoa ni pamoja na kuwapa unafuu wachimbaji wadogo wadogo wa na wakati wa madini kwa kununua mashine na gari kwa malipo ya kidogo kidogo huku wakitanguliza nusu kama malipo ya awali.
"Ndugu katibu mkuu karibu sana kwenye banda letu tuko hapa kwa ajili ya kuwahudumia wanaanchi hivyo na sisi tumekuwa semehamu ya wadhamini katika kipindi hiki hivyo tunaishukuru serikali ya awamu ya sita kupitia wizara ya madini kututhamini na kuona mchango wetu", amesema.
Amesema kampuni ya GF TRUCK GROUP kwa kipindi hiki cha maonyesho ya tano ya kitaifa ya tekinolojia ya madini 2022 mkoani Geita tumekuja na gari pamoja na mashine aina ya Excavator Xe 215c kwaajili yashughuli za uchambaji madini", amesema Deus.
Deus ameongeza kuwa pamoja na yote pia watafanya shughuli za kuchangia damu kwa kushirikiana na damu salama na zoezi hilo litakwenda sambamba na utoaji wa zawadi kwa watu watakaojitokeza kuchangia damu kwenye viwanja hivyo vya maonyesho vya Bombambili.