Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ADAKWA TUHUMA ZA KUMUUA MWANAMKE NA KUMTUPA KATIKA SHAMBA LA MITI




Jeshi la polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Kifanya kitongoji cha Muungano kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwanamke ambaye utambulisho wake haujajulikana anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25-28 aliyekutwa amefariki kwenye shamba la miti.

Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issa anasema hadi sasa mwili wa mwananke huyo umehifadhiwa katika hospitali ya mji Njombe Kibena na kisha kutoa rai kwa wananchi Kwenda kuangalia mwili huo ili uchukuliwe na ndugu.

Katika hatua nyingine Kamanda Issa amewataka wamiliki wa shule binafsi kupeleka mara moja mabasi yanayobeba Watoto kukaguliwa ili kulinda usalama wao wa watoto.
                               

                             CHANZO-EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com