Katibu mkuu wa michezo nchini Rwanda Didier Shema Maboko, amesimamishwa kazi na Rais wa nchi hiyo Paul Kagame.
Taarifa kutoka kwa waziri mkuu nchini humo Bw. Edouard Ngirente haikuweka wazi sababu za kusimamishwa kazi kwa kiongozi huyo ambaye amesimama kazi mara moja kuanzia jana.
Maboko ameitumikia nafasi hiyo kwa karibia miaka mitatu sasa tangu alipochaguliwa mwezi Novemba 2019.
Amekuwa akifanya kazi kadhaa kwenye sekta ya micheo nchini humo ikiwemo mkurugenzi wa ufundi katika shirikisho la mpira akikapu la Rwanda FERWABA.
Makobo amewahi kuwa mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu.
Social Plugin