Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili.
Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao, wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili.
Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Meatu, Bw. Msoleni Dakawa, akitoa taarifa ya utelezaji wa majukumu ya halmashauri yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (Wakwanza kulia), wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi katika halmashauri hiyo.
Mkuu wa Shule ya Kimali, Bw. Marco Ng’wendamunkono wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu (aliyesimama) akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa halmashauri hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi (Wakwanza kushoto) akijibu hoja iliyokuwa imewasilishwa na mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo. Kulia Kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Fauzia Ngatumbura na kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Oscar Maduhu.
Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Thomas Shishwa akitoa neno la shukurani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi, wakati wa ziara yake ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.
***************************
Na. Veronica E. Mwafisi-Meatu
Tarehe 28 Septemba, 2022
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka watumishi wa umma nchini kujituma na kujitoa kikamilifu katika kuwahudumia wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zinazotolewa na Serikali kupitia taasisi zake.
Mhe. Ndejembi ametoa wito huo kwa watumishi wa umma, wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu akiwa katika ziara ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamozo zinazowakabili watumishi wa umma katika Wilaya hiyo.
Mhe. Ndejembi amesema, watumishi wa umma ni mabalozi wa serikali hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu, weledi, kujituma na kujitoa kwa ajili ya serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
“Mtumishi wa umma ni mwakilishi wa serikali mahali anapofanya kazi, hivyo hana budi kutambua kuwa serikali imemuajiri ili kuwatumikia wananchi kwa kuwapatia huduma bora kama ambavyo serikali imekusudia,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Meatu, Bw. Msoleni Dakawa amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ajira mpya 104 katika Halmashauri hiyo zikiwemo kada za elimu na afya ili kuwahudumia wananchi wilayani humo.
Aidha, Bw. Msoleni ameishukuru ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kutoa kipaumbele cha kuwapatia stahiki watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.
Naye, Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Thomas Shishwa kwa niaba ya watumishi wengine, amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kutenga muda wake kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi papo kwa hapo, ikiwa ni pamoja na kuwapatia ufafanuzi wa hoja za masuala ya kiutumishi walizoziwasilisha.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi anaendelea na ziara ya kikazi Mkoani Simiyu yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani humo.
Social Plugin