















(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
**************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la bima la Taifa (NIC) limekabidhi shilingi Milioni 40 kwaajili ya kuiunga mkono timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) pamoja na timu ya taifa ya Walemavu (Tembo Warriors National Team) pamoja kutoa bima zitakazowalinda wakipata majanga wakati wakiwa nje ya nchi.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga Serengeti Girls leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa ameipongeza NIC kwa kuamua kushiriki kwa namna moja katika kusaidia timu hiyo kwenda kufanya vizuri katika michuano ya kombe la Dunia.
Aidha amewataka wachezaji wakapambane na kuweza kufanya vizui kwenye michuano hiyo kwani uwepo wa bima hiyo itaweza kuwasaidia pindi wanapopata changamoto katika michezo waweze kusaidika kwa urahisi na kwa haraka.
Hata hivyo amewataka wachezaji hao kuwa wazalendo wa nchi yao kwa kuhakikisha wanapambana na kufanikiwa kufanya vizuri kwenye michuano hiyo ambayo inatarajia kufanyika hivi karibuni.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw.Elirehema Doriye amesema kuwa kwa wale wachezaji watakaoumia kila wiki watakuwa wanapewa laki moja kwa kipindi ambacho amekaa mpaka kufikia milioni 10, hivyo amewataka wachezaji hao kupambana na wasiogope kuumia.
Amesema timu hiyo ikifanya vizuri na kufika hatua ya robo fainali, watazawadiwa kiasi cha shilingi milioni 40, wakifika nusu fainali watawazawadia shilingi milioni 80 na wakifika hatua ya fainali watapatiwa milioni 100.
"Mnatakiwa mkapambana na kuhakikisha mnaipeperusha vizuri bendera ya Tanzania, mkafanye vizuri na msigope kuumia hata hivyo ikitokea imchezaji akapata kilema cha kudumu atalipwa hivyo basi NIC ipo kwaajili yenu na tunawatakia kila la heri kwenye michuano hiyo". Amesema Bw.Doriye
Social Plugin