Rajab Masanche akishiriki katika kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Septemba 27,2022
**
Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Rajab Masanche amefariki dunia alfajiri ya leo, Jumatano Septemba 28, 2022.
Jana Septemba 27,2022 Masanche alishiriki katika kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga.
Kikao hiko kilipitia na kujadili Tarifa ya Hesabu za Mwaka za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga katika mwaka wa fedha 2021/2022.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Jomaary Satura amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rajab Masanche huku akibainisha kuwa halmashauri hiyo imepoteza mfanyakazi mahiri.
“Amefariki tu ghafla, jana alikuwa mzima aliendesha baraza la madiwani kama kawaida, akakagua miradi ya maendeleo kisha akaenda nyumbani kupumzika ,ilivyofika usiku akaanza kujisikia vibaya akakimbizwa hospitali akafariki dunia. Vipimo vya madaktari vimeonesha alikuwa anasumbuliwa na Nimonia…Mungu ailaze mahali peponi roho ya marehemu Rajabu Masanche. Amina”, amesema Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Satura.
Social Plugin